Searching...
Ijumaa, 19 Julai 2013

BIFU KALI LAIBUKA KATI YA JANUARI MAKAMBA NA JOHN MNYIKA,ZITO AWASHANGAA-NANI MTETEZI WA KWELII?

JANUARY MAKAMBA AKISALIMIANA NA WANANCHI. 
John Mnyika kaweka namba yangu ya simu ya mkononi ili watu wanipigie na kutukana. Nadhani ni siasa isiyo ya kistaarabu. Hadi sasa nimepata messages zaidi ya 600. Sio sahihi kabisa.
Wabunge WOTE tulishindwa kupitisha maamuzi yenye maslahi kwa mtu wa kipato cha chini. Harakati za mitandaoni haziondoi ukweli huo. Vilevile, kodi hii imepitishwa tarehe 29 Juni 2013.  
JOHN MNYIKA.
Kwa Mbunge ambaye alikuwa na wajibu wa kulipinga siku hiyo na kulisemea kuanzia tarehe 30 Juni 2013 kuamka leo na kutapatapa mitandaoni ni unafiki mkubwa na ni siasa za kuangalia upepo unapovuma na ni unafiki mkubwa. Namheshimu Zitto Kabwe kwasababu alitoa kauli immediately ya kusema anaona aibu kuwa sehemu ya Bunge hili na kwamba wawakilishi wa wananchi wamewaangusha wananchi. Mwenzake John Mnyika anajitoa fahamu na kufanya harakati kupitia press releases.
Suluhisho hapa sio kulumbana wala kutupiana lawama. Suluhisho ni kurudi Bungeni na kubadilisha pale tulipokosea. Sio kutafuta umaarufu mitandaoni. Kunapotokea kosa, tunasahihisha haraka then we move on. Siasa sio kwenye kila jambo.
 
ZITO KABWE NA JANUARY MAKAMBA.
#‎SIMCARDTAX Inaweza kuleta ukakasi katika namna tunavyotazamana. Napenda kuweka hapa tweets zangu za tarehe 4 Julai ambazo ziliujulisha Umma kuhusu kodi hii. Pia nilitaka wananchi wajitokeze kuipinga. Nilisikitika sana kuwa kwetu kimya katika suala hili linalohusu wanyonge.
Ifahamike, kipaumbele changu ni kodi hii kufutwa kutokana na nguvu ya wananchi wenyewe. Nilipoomba wanasiasa wenzangu vijana ndugu John Mnyika na ndugu January Makamba kuepuka kurushiana maneno, lengo langu ni kuhakikisha 'we dont lose focus' from real issue. Real issue here is the rudimentary simcardTax. Our focus shall be to repeal it asap. Mengine mbwembwe tu......
Zifuatazo ni Twits za Zitto kwa watanzania kuhusu kodi ya kadi za simu
Zitto Zuberi Kabwe @zittokabwe 4 Jul
Kodi ya tshs 1000 kwa mwezi Kwa kila kadi ya simu uliyonayo imeanza rasmi. Bunge la wananchi, wawakilishi wa... http://fb.me/2vREC81sO
Expand
Zitto Zuberi Kabwe @zittokabwe 4 Jul
@aeyakuze ndio. Naona aibu sana kuwa mbunge hivi sasa. Tena mbunge wa upinzani. Naona aibu zaidi kuwa hatusemi haya ya wanyonge @jmakamba
View conversation
Zitto Zuberi Kabwe @zittokabwe 4 Jul
@DeoKillian Hapana. Wabunge tunatumia muda mwingi sana kuzungumzia siasa bungeni kuliko masuala ya wananchi wanyonge
View conversation
Zitto Zuberi Kabwe @zittokabwe 4 Jul
@Semkae yaani muuza mihogo barabarani analipa tshs 1000 kila mwezi kodi ya simucard sawa na Mbunge mwenye kipato cha zaidi ya tshs 11m/mwz
View conversation
Zitto Zuberi Kabwe @zittokabwe 4 Jul
@Semkae nashangazwa sana na kimya hiki wakati tunaumiza wanyonge. Kodi ya simcard is very rudimentary way of collecting taxes. Regressive
View conversation

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!