Searching...
Ijumaa, 19 Julai 2013

WATU WANNE WAFARIKI DUNIA KATIKA AJALI MBAYA YA BASI JIONI HII HUKO MKOANI DODOMA.

Watu wa nne wamefariki dunia papo hapo na wengine wengi kujeruhiwa baada ya basi walilokuwa wakisafiria kutoka jijini DSM kwenda Mkoani mwanza la kampuni ya NAJIMUNISA kupinduka eneo la mbande wilayani Kongwa mkoani dodoma.
Kwa mujibu wa taarifa iliyorushwa hewani muda huu na kituo cha radio one stereo zinasema chanzo cha ajali hiyo ni kupasuka kwa tairi la mbele wakati basi hilo likiwa katika hali ya mwendo kasi na hivyo kumshinda dereva na kisha kupinduka.
Endelea kufuatilia MCHOME BLOG Kwa taarifa zaidi na picha za ajali hiyo muda mfupi ujao.
MWENYEZI MUNGU AZILAZE MAHALA PEMA PEPONI ROHO ZA MAREHEMU NA KUWAPONYA HARAKA MAJERUHI WA AJALI HIYO AMEEEEEN!!!!

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!