Searching...
Jumanne, 23 Julai 2013

HAYAWI HAYAWI...ROONEY ACHEZA GOLF UWANJA WA CHELSEA.

Wayne Rooney WAYNE ROONEY AKICHEZA GOLF MITA 100 KUTOKA MAKAO MAKUU YA CHELSEA.
Mchezaji wa nafasi ya ushambuliaji wa Manchester United Wayne Rooney ambaye kwa sasa hayupo pamoja na kikosi chake kutokana na madai ya kuwa majeruhi jana ameonekana akicheza golf karibu kabisa na makao makuu ya klabu ya Chelsea ambayo inamuwania kwa udi na uvumba 
Klabu ya Chelsea wiki iliyopita ilishindwa kuishawishi klabu ya Manchester United Kumsainisha mshambuliaji wao nguli kwa kitita cha paundi milioni 20 ambaye kwa sasa hana amani ndani ya klabu hiyo
Rooney alirejeshwa nyumbani na kuwaacha wenzake wakiendelea na ziara ya kujiandaa na msimu ujao wa ligi huko Asia na Australia kutokana na majeraha aliyoyapata katika siku mbili za awali za katika ziara hiyo lakini pamoja na kwamba sasa yupo fiti hajaenda kujiunga na wenzake katika ziara yao hiyo inayoendelea na badala yake amesafiri hadi London karibu kabisa na makao makuu ya Chelsea na kucheza golf na timu ya  Queenwood Golf Club uwanja ambao pia hutumiwa zaidi na nyota wa chelsea kuchezea golf kiashiria ambacho kinaonyesha wazi kwamba Rooney sasa akili yake yote ipo Stamford Brige na sio Old Trafford.
David Moyes wants to keep Rooney at Old Trafford David Moyes kocha wa Manchester United ameapa kwamba Rooney hauzwi kwa dau lolote na ataendelea kusalia Old Trafford hadi msimu ujao uishe licha ya kwamba hayumo kwenye kikosi chake cha kwanza.
Jose Mourinho said last week it was 'Rooney or bust' as far as he was concerned Jose Jose Mourinho kocha wa Chelsea ameapa kwamba ni lazima Rooney avae uzi wa Blue msimu ujao bila kujali anao mkataba na Man U kwani sheria zinaruhusu kuvunja mkataba ilimradi mchezaji mwenyewe aridhie na uwe na uwezo wa kulipia uvunjaji wa mkataba.
Rooney had been part of United's pre-season tour Wayne Rooney ambaye anawapasua kichwa Moyes na Mourinho na ambaye ameonyesha wazi wazi kwamba hataki tena kuichezea Man U na kuonyesha hisia zake za kutua Chelsea.
Chelsea are currently in the middle of their pre-season tour of Asia Hiki ndicho kikosi kamili cha Chelsea ambacho kinaendelea na ziara yao huko mashariki ya mbali kujiandaa na msimu ujao wa ligi kuu England.

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!