Wajukuu wa Malkia Elizaberth WILLIAM & CATHERINE ambao wanatarajiwa kukabidhiwa kijiti cha kuiongoza England kama Mfalme na Malkia ambao usiku wa kuamkia leo wamepata mtoto wa kiume ambaye amepewa nafasi ya tatu kutoka sasa kuwa Mfalme wa England,hawa walioana April 2011 na taarifa za Catherine kuwa mjamzito zilitangazwa mwezi December 2012.Hapa bwana mkubwa akitangaza tangazo la kuzaliwa kwa mwana wa MfalmeHii ni taarifa rasmi ya serikali ikieleza kuwa mjukuu wa Malkia Elizaberth amejifungua mtoto wa kiume saa 4.24 pm jana kwa saa za Uingereza na wote mama na mtoto wanaendelea vizuri.Hawa ni maelfu ya waingereza waliofurika katika kasri la kifalme la Buckingham Palace kusherehekea kuzaliwa kwa mfalme wao ajaye.
Baada ya mamilioni ya waingereza kusubiri taarifa za mtoto kuzaliwa hatimaye muda ulifika na Huu ni mnara wa mawasiliano wa England ukiwapa waingereza taarifa kwamba mtoto kazaliwa na IT'S A BOY kama unavyoona mwenyewe hapo.
Hapa waingereza wakiendelea kunyeshewa na Mvua bila kujali wakiwa nje ya jumba la kifahari la mfalme maarufu kama Buckingham Palace wakiendelea kusherehekea kuzaliwa kwa mfalme wao wa baadae.
Ujumbe wa heri njema umeendelea kutolewa kutoka kote
duniani baada ya Kate na Prince William ambaye atakuwa wa tatu kwenye
foleni katika kurithi ufalme wa Uingereza.
Mwanamfalme William na mkewe Kate ,wameamkia
hospitalini asubuhi ya leo mjini London baada ya kupata mtoto wao wa
kwanzaJumatatu jioni.
Mtoto huyo aliyezaliwa akiwa na takriban kilo tatu na nusu atafahamika kama........
mwanamfalme wa Cambridge, lakini hajapewa jina.
Katika taarifa fupi William,amesema wana furaha isiyo na kifani.
Baadaye leo jeshi la Uingereza linatarajiwa
kutoa heshima kwa kuzaliwa mwanamfalme huyo kwa kurusha mizinga 40
hewani huko London na kengele la kanisa la Westminster Abbey zitalia.
Kawaida saluti ambayo hutolewa kwa mwanamfalme
huwa ni mizinga ishirini na moja lakini huongezeka hadi arobaini na moja
ikiwa itarushwa kutoka katika makao ya kifalme
Taarifa kutoka katika Kasri la Buckingham,
zinasema kuwa Malkia Elizabeth na mumewe walifurahishwa sana na habari
za kuzaliwa kwa mtoto huyo. Naye babake William
Prince Charles, alisema ana furaha isiyo kifani na ana raha sana kuwa babu kwa mara ya kwanza.
Prince Charles, alisema ana furaha isiyo kifani na ana raha sana kuwa babu kwa mara ya kwanza.
Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron, alisifu sana kuzaliwa kwa mtoto huyo na kuitaja kuwa hatua muhimu sana kwa Uingereza.
Naye wawiri mkuu wa Australia, Kevin Rudd,
alitaja sherehe za jana kama muhimu sana kwa nchi za juimuiya ya madola,
huku akiongeza kuwa watu wa Australia wanampenda sana Prince William
baada ya kuzuru nchi hiyo akiwa mtoto mwenyewe.
0 comments:
Chapisha Maoni