Searching...
Jumapili, 14 Julai 2013

...MSHTUKOOOOOOOO!!!!HATIMAYE SASA MFALME DROGBA KUREJEA DARAJANI CHELSEA BILA UBISHI


I want Blue! Drogba had a private chat with Jose Mourinho earlier this week
Gazeti la England la Sunday Mirror limetoboa siri kwamba mchezaji huyo wa Ivory cost kipenzi cha Mourinho alikua kwenye uwanja wa mazoezi wa Cobham jumatatu iliyopita na kuzungumza na Mourinho japo yalikua ni mazungumzo ya siri kali kati ya wawili hao.
Inafahamika kwamba Mourinho anataka kuwashangaza wengi kumrudisha Drogba Chelsea msimu huu lakini kwanza ni lazima wazungumze uzuri na klabu yake ya sasa ya Galatasaray.
Ila kama klabu hiyo ya Uturuki itamzuia Drogba kuondoka basi itamlazimu Mourinho kusubiri hadi hapo mwakani Drogba atakapomaliza mkataba wake na klabu hiyo na kumpa mkataba mfupi wa miezi 12

Chelsea manager Jose Mourinho with Didier Drogba (r) and his man of the match award
Mmiliki wa klabu ya Chelsea tajiri Roman Abramovich alijaribu kumrudisha Drogba mwezi January kwenye usajili wa dirisha dogo lakini ikashindikana lakini sasa kwa msukumo wa Mourinho ameapa kumrudisha kwa gharama yoyote ile.
katika heka heka za kurejea Chelsea Drogba mapema mwaka huu amekaririwa akisema “Itakuwa vizuri sana kurejea Chelsea,sio kwaajili ya kuifundisha bali kuisaidia timu.
“Kwa Chelsea nimewapa kila kitu na wao pia wamenipa mambo mengi,huwa mara zote nikienda England najisikia nipo nyumbani”

Didier Drogba is lifted by teammate Frank Lampard #8 after scoring a goal against AC Milan during the Championsworld SeriesWiki iliyopita,Mourinho alizungumza kuhusu uwezekano wa kumjumuisha Drogba kwenye kikosi chake“Ninaweza kumtumia Drogba kwenye kikosi changu kama njia ya kuwashawishi wachezaji chipukizi kunifuata mimi kwani Didier amekua akinifuata tangu siku ya kwanza”
Mourinho ndiye aliyemsajili Drogba Chelsea ambaye pia ni mchezaji wa kimataifa wa Ivory Coast na kuifungia magoli 157 katika kipindi cha miaka nane aliyodumu na klabu hiyo.

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!