Arsenal wamemtolea uvivu Gonzalo Higuain kwamba wanahitaji maamuzi ya haraka kama anahitaji kujiunga na wabeba bunduki hao wa England msimu ujao au waangalie mbadala wake,Arsenal wamekuwa na mazungumzo na klabu ya Madrid pamoja na mchezaji mwenyewe mwezi mzima sasa lakini inaonekana kama yupo mguu mmoja ndani na mwingine nje
Sasa mzee Arsene Wenger amechoka na ameamua kuweka wazi kama Higuan ana mpango wa kutua Emitates na kula mshahara wa paundi 150,000 kwa wiki au aangalie mchezaji mwengine.
0 comments:
Chapisha Maoni