Searching...
Jumanne, 2 Julai 2013

...BREAKING NEWZZZZZZZZZ!!!!! WATU 21 WAJERUHIWA VIBAYA KATIKA AJALI YA SAIBABA ASUBUHI YA LEO,30 WANUSURUKA

Habari ambazo zimetufikia hivi punde kupitia mtandao huu wa MCHOME BLOG zinasema watu 21 wamejeruhiwa vibaya na wengine 30 wakinusurika kifo baada ya basi walilokuwa wakisafiria kutoka jijini Dar es salaam kwenda Songea kupata ajali eneo la vigwaza mkoani pwani.
 akizungumza na MCHOME BLOG mkuu wa kikosi cha askari wa barabarani Chalinze Assistance Inspector Sule amesema ajali hiyo imetokea majira ya saa mbili asubuhi ya leo baada ya basi la abiria la kampuni ya Saibaba lenye namba za usajili T 779BKL kutaka kulipita gari lingine huku likiwa katika mwendo kasi na hatimaye gari lilimshinda dereva huyo na kisha kupinduka
Aidha ameongeza kuwa majeruhi hao wamekimbizwa katika hosiptali ya tumbi kibaha kwaajili ya matibabu,basi hilo lilikuwa na jumla ya abiria 51.

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!