Searching...
Ijumaa, 19 Julai 2013

PIGO KUBWA BARCELONA-KOCHA WAO TITO VILANOVA KUJIUZULU USIKU HUU.

Vilanova 'to announce imminent Barcelona resignation'TITO VILANOVA-KOCHA WA BARCELONA ANAYEJIUZULU USIKU HUU.
Kocha mkuu wa Barcelona na kipenzi cha wachezaji,viongozi na mashabiki wa klabu hiyo ya Hispania
Tito Vilanova anatarajiwa kutangaza rasmi kujiuzulu nafasi hiyo mbele ya waandishi wa habari usiku huu kutokana na kuendelea kusumbuliwa na ugonjwa wa saratani
Mabingwa hao wa soka nchini Hispania maarufu kama Catalan wameitisha mkutano na waandishi wa habari utakaofanyika saa 19:30 usiku  huu  kwa saa za huko ambapo imeelezwa kwamba lengo au madhumuni ya mkutano huo ni kutangaza kujiuzulu kwa kocha wao Tito Vilanova ,nafasi yake inatarajiwa kuchukuliwa na kocha Joan Francesc Ferrer Sicily kama kocha wa muda wakati wakiendelea na mazungumzo ya kumpata kocha wa kudumu.
kocha Vilanova,ambaye ameonyesha mafanikio makubwa ya kuiongoza klabu hiyo baada ya kumrithi  Pep Guardiola Nou Camp msimu uliopita ameiongoza Barca kuchukua kombe la ligi kuu ya hispania maarufu kama La Liga na kuwafikisha hatua ya nusu fainali katika mashindano ya klabu bingwa ulaya maarufu kama  Champions League.
Lakini maisha yake ya baadae ndani ya klabu hiyo yamekuwa tatani baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa saratani.Vilanova 'to announce imminent Barcelona resignation'
Msaidizi wake Jordi Roura alichukua nafasi ya Vilanova kipindi chote alipokuwa kwenye matibabu mapema msimu uliopita lakini alirejea mwezi wa tatu mwaka huu baada ya matibabu na kuendelea na nafasi yake hadi mwishoni mwa msimu uliopitatoo,Mashabiki na wachezaji wameonyesha masikitiko yao kufuatia hali ya afya ya kocha wao ambayo sasa inamlazimu kuachia ngazi rasmi usiku huu.

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!