Wanafunzi
117 wa Polisi, wamefukuzwa katika Chuo cha Taaluma na Mafunzo ya Polisi
(MPA), kilichopo Manispaa ya Moshi, mkoani Kilimanjaro.
Waliotupiwa virago na kufutwa kwenye kozi hiyo ni wale waliopoteza sifa za kuendelea na mafunzo ya kijeshi baada ya kukutwa na makosa ya utovu wa nidhamu, utoro na matatizo ya kiafya.
Kamishna
Msaidizi wa Polisi (ACP), Matanga Mbushi, ambaye ni mkuu wa chuo hicho
aliliambia NIPASHE katika mahojiano maalumu kwamba, waliotimuliwa chuoni
ni.......Waliotupiwa virago na kufutwa kwenye kozi hiyo ni wale waliopoteza sifa za kuendelea na mafunzo ya kijeshi baada ya kukutwa na makosa ya utovu wa nidhamu, utoro na matatizo ya kiafya.
kati ya askari wanafunzi 3,189 waliokuwa wamesajiliwa kuanza mafunzo ya kijeshi katika chuo hicho, Oktoba 25 mwaka jana.
Kati
yao askari 115 ni wale wa Polisi na askari wawili wanatoka katika Idara
ya Uhamiaji iliyopo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani.
Kufukuzwa
kwa wanafunzi hao , kuna akisi moja kwa moja jinsi menejimenti ya chuo
hicho ilivyojipanga upya kupunguza wimbi la baadhi ya askari walioko
kazini na ambao wanalipaka matope jeshi hilo kutokana na kupotoka
kimaadili kwa kutaka kujinufaisha kimaslahi.
Askari
hao walikuwa waungane na wenzao ambao wanatarajiwa kuhitimu mafunzo ya
awali ya polisi na uhamiaji, Julai 26 mwaka huu baada ya kupatiwa
mafunzo ya medani za kivita.
Mgeni wa heshima atakayeshuhudia kuagwa kwa askari 3,092 ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi.
Kamishna
Mbushi alisema askari hao pamoja na mambo mengine wamepatiwa mafunzo
maalumu ya utunzaji wa amani ya nchi iliyopo, Teknolojia ya Habari na
Mawasiliano (ICT), Haki za Binadamu, Masuala ya mtambuka (Cross cutting
issues), Usimamizi wa majanga na Usimamizi wa kazi za Polisi.
Mafunzo
mengine ni pamoja na Polisi Jamii, Sheria ya ushahidi, Sheria ya
mwenendo wa makosa ya jinai, Upelelezi wa makosa ya jinai, Usalama
barabarani na stadi za kazi.
Taarifa
za awali kutoka ndani ya chuo hicho, zinaeleza kuwa mahafali hayo ya
Polisi yatatanguliwa na medani za kivita yatakayofanyika Julai 25 huko
katika Kijiji cha Kilele-Pori, Wilaya ya Siha.
Chanzo:Nipashe.
0 comments:
Chapisha Maoni