Searching...
Jumanne, 11 Juni 2013

JESHI LA POLISI KWA KUSHIRIKIANA NA ASKARI WA HIFADHI ZA TAIFA TANAPA MKOANI KIGOMA WAKAMATA SILAHA ZA KUTISHA KWA WANANCHI

Jeshi la polisi mkoani Kigoma, kwa kushirikiana na Hifadhi za Taifa kanda ya magharibi , wamekamata bunduki 22 , risasi na nyara za serikali katika oparesheni ya pamoja ya kupambana na majangili katika hifadhi pamoja na wahalifu inayoendelea katika mkoa wa kigoma .

kamanda wa polisi mkoa wa kigoma Fraisser Kashai amesema katika oparesheni hiyo inayoendelea katika vijiji vilivyo jirani na hifadhi , zimekamatwa bunduki ishirini zilizotengenezwa kienyeji aina ya gobore pamoja na short gun mbili , silaha ambazo zilikuwa zikitumiwa kwa ujangili wa wanyama katika hifadhi na uhalifu ikiwa ni pamoja na utekaji magari na kwamba watuhumiwa 23 wamekamatwa na wanatarajiwa kufikishwa mahakamani
kwa upande wake mkuu wa hifadhi ya taifa ya milima ya mahale wilayani uvinza bw.  herman batio   amesema hali ya ujangili katika hifadhi ni mbaya kutokana na kuwepo kwa idadi kubwa ya watu kujihusisha na ujangili na hivyo kuathiri wanyama na ikolojia katika hifadhi ambapo amewaomba wananchi wanaoishi jirani na hifadhi kutoa ushirikiano ili kudhibiti hali hiyo

 Picha na habari kwa hisani ya DEOGRATIUS NSOKOLO Kigoma

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!