|  
     Msanii
 wa Muziki wa Kizazi,Kala Jeremiar akitoa shukrani zake kwa mashabiki 
waliompigia kura na kumuwezesha kupata Tuzo tatu zikiwa ni Msanii Bora 
wa Hip Hop,Mtunzi Bora wa Mashairi ya Hip Hop pamoja na Wimbo Bora wa 
Hip Hop kwa kipindi chote cha Mwaka 2012/13.Kulia ni Msanii Shilole 
aliepanja jukwaani Kumsindikiza.Hafla hii ya utoaji tuzo imefanyika 
Usiku wa kuamkia leo kwenye Ukumbi wa Mlimani City,jijini Dar es Salaam. 
     Msanii
 Mkongwe wa Muziki wa Hip Hop hapa nchini ambaye sasa amepotea kidogo 
kwenye Gemu hilo,Gwamaka Kaihula a.k.a King Crezy G.K akiwasalimia 
mashabiki wake pindi alipopanda jukwaani kutoa tuzo ya Msanii Bora wa 
Hip Hop. 
DJ 
Mseto toka Citizen TV ya Kenya akimuwakilisha mwanamuziki Jose 
Chamilione baada ya kupata tuzo ya Wimbo bora wa Afrika Mashariki. 
Ommy Dimpoz kwa Pozi aliondoka na tuzo tatu usiku wa kuamkia leo pale Mlimani City,jijini Dar 
Mkurugenzi
 wa Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),Kushila Thomas (katikati) 
akiwa katika picha ya pamoja na kiongozi wa Bendi ya The Kilimanjaro 
(wana njenje),Waziri Ally pamoja na Mwana FA baada ya kukabidhi tuzo ya 
heshima kwa bendi hiyo,wakati wa hafla ya utoaji tuzo kwa wanamuziki 
mbali mbali iliyofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye Ukumbi wa Mlimani 
City,jijini Dar es Salaam. 
Mkurugenzi Mkuu wa Konyagi,David Mgwassa (kushoto) akikabidhi tuzo  
Redd's
 Miss Tanzania 2012,Brigit Alfred akikabidhi tuzo ya Msanii Bora wa Kike
 iliyokwenda kwa Bint Komando Lady Jay Dee.Anayeipokea tuzo hiyo ni 
Mumewe Lady Jay Dee,Ndugu Garder Habash. 
G. Habash akizungumza kwa niaba ya Lady Jay Dee. 
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager,George Kavishe akitangaza mshindi wa tuzo Msanii Bora wa Bongo Flava. 
Muwakilishi wa Msanii Diamond akishukuru kwa niaba yake. 
Mtunzi Bora wa Mashairi ya Muziki wa Taarab ni Thabit Abdul na hapa akipongezwa. 
Khareed Chokoraa akichukua tuzo ya Msanii Bora wa Kike,ambayo ilikwenda wa Mkongwe Khadija Kopa. | 
Jumatatu, 10 Juni 2013
          Related Posts
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)











 
 
0 comments:
Chapisha Maoni