CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wilayani Kyela mkoani Mbeya kimejipanga kujiimarisha zaidi vijijini kwa kuelekeza nguvu zaidi katika maeneo hayo


Akizungumza na mwandishi wa habari hizi katibu wa CHADEMA wilayani Kyela Bw,Mwiteni Mohamed alisema kuwa hivi sasa ajenda kubwa ndani ya chama hicho ni kufanya ziara katika kata zote 20 na kuwa zoezi hilo wamelianza toka Mei 25 na linatarajia kumalizika juni 30 mwaka huu


Alisema kuwa ziara hiyo imewasaidia kuweza kukutana na wanachama na kuweza kuzungumza kupitia mikutano ya ndani na ile ya nje  na kuwa imewasidia sana kujua uhai ndani ya chama na kufanya jitihada za kufufua chama baadhi ya maeneo ambayo yalionyesha udhaifu


Katibu huyo wa wilaya alifafanua kuwa hivi sasa chama hicho kipo kwenye mafunzo ya mpango mkakati wa M4C sambamba na sensa ya wanachama wote kwa lengo la kutaka kujua idadi ya wanachama kuanzia ngazi ya matawi na willaya


Pia chama hicho kimejikita zaidi katika kutoa elimu ya uraia kwa jamii  ya kujua haki zao za msingi zitakazowawezesha kudai na kuweza kujiletea maendeleo


Ziara hizo ambazo lengo ni kuifikia wilaya nzima ya Kyela zinaongozwa na madiwani wa chama hicho sambamba na viongozi wa chama hicho,katika ziara hiyo makada 78 wa ccm wamejiunga na chadema huku kadi za ccm wakizichoma moto.
NA IBRAHIM YASSIN