Searching...
Jumatano, 5 Juni 2013

ANGALIA AIBU YA MWAKA TFF,MAGARI YACHUKULIWA KWA NGUVU KISA DENI LA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 51

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjIH7E5DRYS-8yKL5HOEQmhwp1zQcNi8Ms67vWvzZ_NIKhNEanubF8A6wFXV4JA374pRCcZlKp4byVYZF2sM6qk7ApS2PEQ8V8niBMN3PzMd8lku5UAelVryFhAdGe00NMJOXvYInV9WFQ/s1600/download+(5).jpg
 Basi la TFF likipigwa Tanganyika jeki ya nguvu
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiO-18lcxTEI3jfOE-aysQv_Ay9Z3ajZGNaIdoBoQeNtylc9SyDOmsesZTpxGDunfG6J29CNJJuycS2gOnC9hb_zgBwD0K58DCWmtFfYy4A8e0RnAMDF7zGYtGG1qMs2JUQPzgzIrUlxgg/s1600/kuzuia+gari+zisitoke+(4).JPG
 Magari binafsi ya maofisa wa TTF yaliegesha getini kuzuia mabasi ya TFF yasichukuliwe
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg4cI34HOfmRlqov8o8ZLfWzWDweptZ55Hv_WOZ50NmUn2I1kFgIaoz_gEOJYfGrKfu_Rajntw-vLYDdZFlQjgL1qXpBewE0kdxXBgLB_-uEbyknT4KKUzwSIj43VQXwS54jxSmm9FbQbM/s1600/download+(1).jpg
Katibu mkuu wa TFF Angetile Hosea akizungumzia aibu hiyo
=================
 
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) leo wamejikuta wakipata aibu ya mwaka baada ya Kampuni ya  Flamingo Auction Mart, kuyapiga tanganyika jeki mabasi ya shirikisho hilo kutokana na deni la zaidi ya  Sh.50 milioni la Kampuni ya Safina Holding ya jijini Dar es Saalam.

Kampuni hiyo ya Flamingo leo ilitia timu kwenye ofisi za shirikisho hilo kufuatia amri ya Mahakama ya  Hakimu Mkazi Kinondoni ikitaka zoezi la ukamataji magari hayo hadi Juni 30 liwe limeshakamilika.
 
Fedha hizo za Safina Holding zimetokana na hifadhi ya baadhi ya timu zilizoshiriki michuano ya Kombe  la Kagame mwaka jana na Yanga kuibuka kidedea.

Magari ambayo yameamriwa na mahakama hiyo kukamatwa ni basi aina ya Yutong lenye namba za usajili
T 581 CGR pamoja na Toyota Mini Bus lenye namba za usajili T 528 ASJ.


Lakini tofauti na amri hiyo ya Mahakama maofisa hao wa Flamingo walijikuta kwenye wakati mgumu  baada ya kuingia kwenye mzozo na maofisa wa TFF na kuzuka zogo kubwa huku maofisa hao wa TFF  wakiongozwa na Katibu mkuu Angetile Osiah kuzuia magari hayo yasichukuliwe.

Maofisa hao wa Flamingo wakiongozwa na Meneja Operation wao Noel Nyalila walitinga kwenye ofisi  hizo na kulifunga gari lenye namba za usajili T 528 ASJ aina ya Coster na kulivuta kwenye gari lao lenye  namba T 972 ABJ Jay Ambe, lakini walishindwa kuondoka nalo baada Osiah kuwaogoza wafanyakazi  wake kuzuia kwenye geti.

Wafanyakazi hao wa TFF waliamua kuzuia kwa kuegesha magari yao binafsi yenye namba T 643 BJW na  lingine lenye namba T 507 BER, hivyo kuzuia magari yaliyoamriwa kuchukuliwa.

Akizungumza kwa hasira Osiah alisema wamelazimika kuzuia magari yao kuchukuliwa kutokana na  utata wa tarehe iliyioandikwa kwenye amri hiyo ya Mahakama, ambayo alidai kuwa inaonyesha kwamba  inapaswa kutekelezwa Juni 31 mwaka huu.

“ Tumelazimika kuzuia kwa sababu mwanasheria wetu amekwenda mahakamani ili kupata udhibitisho  wa amri hii, kwa sababu tarehe ya kukamata magari haya ambayo ni Coster yenye namba T 528 ASJ na  basi lenye namba T 581 CGR ni kweli tunadaiwa lakini tuna mpango wa kulipa,” alisema Osiah.

Kwa upande wake Meneja Noel alisisitiza kwamba amri hiyo ni halali na wamefika hapo ili kuitekeleza  kwa kuwa hukumu ilitolewa April 23 mwaka huu, amri ikaandikwa Juni 3 mwaka huu, ambapo June 31  wanapaswa kurejea mahakamani. Hata hivyo waliomba msaaa wa Polisi ili waweze kusimamia  kuyachukua magari hayo.

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!