Mkuu wa Mkoa wa
Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akiandika kwenye daftari la mwananfunzi
aliyekaa pembeni yake kama ishara ya matumizi ya madawati 320
yaliyokabidhiwa na taasisi ya Hassan Maajar Trust ya jijini Dar
es Salaam tarehe 06-06-2013 katika shule ya msingi Kasense ikiwa ni
jitihada za taasisi hiyo kusaidia elimu nchini. Mkuu
huyo wa Mkoa aliishukuru taasisi hiyo na kusema mfano wake ni wa kuigwa
ukilinganisha na taasisi zingine ambazo huishia kuilamu Serikali na
huduma zilizopo badala ya kutoa mchango wowote. Kutoka kushoto ni
Mkurugenzi Mtendaji wa Hassan Maajar Trust Bi Zena Tenga na Makamu
Mwenyekiti Ndugu Shariff Maajar. Wa tatu kutoka kushoto aliyesimama ni
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima.
Wanafunzi wa shule
ya msingi Kasense wakiwa wamekalia baadhi ya madawati yaliyotolewa
shuleni hapo na taasisi ya Maajar Trust. Jumla ya shule nane (8) za Mkoa
wa Rukwa kutoka kila Wilaya zenye upungufu mkubwa wa madawati zimepata
madawati arobaini (40) kila moja kuondoa upungufu unaowakabili.
Mkuu wa Mkoa wa
Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akizungumza katika hafla fupi ya
kukabidhi madawati 320 ya taasisi ya Hassan Maajr Trust kwa shule za
msingi Mkoani Rukwa tarehe 06-06-2013 katika shule ya msingi Kasense,
Mkuu huyo wa Mkoa aliishukuru taasisi hiyo na kusema mfano wake ni wa
kuigwa ukilinganisha na taasisi zingine ambazo huishia kuilaumu Serikali
badala ya kusaidia katika huduma za jamii. Aliendelea kusema kuwa
katika kuhakikisha huduma za elimu Mkoani Rukwa zinaboreka atakuwa
dikteta kuhakikisha kila mtu wakiwemo wazazi wanatimiza wajibu wao
katika kuhakikisha huduma za elimu Mkoani Rukwa zinaimarika. Kulia ni
Mkurugenzi Mtendaji wa Hassan Maajar Trust Bi Zena Tenga.
Katibu Tawala Mkoa
wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima akitoa taarifa fupi ya madawati kwa
shule za msingi Mkoani Rukwa katika hafla fupi kukabidhi madawati 320 ya
taasisi ya Hassan Maajar Trust kwa shule hizo Mkoani Rukwa tarehe
06-06-2013 katika shule ya msingi Kasense, Aliishukuru taasisi hiyo na
kusema kuwa Rukwa ina uhaba wa madawati 33,638 sawa na asilimia 50.2%.
Makamu Mwenyekiti wa
taasisi ya Hassan Maajar Trust Bw. Shariff Maajar akizungumza katika
hafla fupi kukabidhi madawati 320 ya taasisi hiyo kwa shule za msingi
Mkoani Rukwa tarehe 06-06-2013 katika shule ya msingi Kasense.
Mwenyekiti huyo alisema kuwa lengo la taasisi hiyo ni kuboresha
mazingira ya kusomea watoto nchini Tanzania. Aliwaasa wadau wa elimu
Mkoani Rukwa kuchangia katika sekta hiyo kwa maendeleo ya taifa.
Mkurugenzi Mtendaji
wa taasisi ya Hassan Maajar Trust Bi. Zena Tenga akizungumza katika
hafla fupi kukabidhi madawati 320 ya taasisi hiyo kwa shule za msingi
Mkoani Rukwa tarehe 06-06-2013 katika shule ya msingi Kasense. Katika
hotuba yake hiyo alisema lengo la taasisi hiyo ni kuboresha mazingira ya
kusomea kwa watoto wa Tanzania na kuhamasisha jamii kutambua wajibu wa
kuchangia ili kuweka mazingira ya shule zetu kuwa mahali bora kwa watoto
kusomea.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hassan Maajar Trust Bi. Zena Tenga akisoma houtuba yake kwenye hafla hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa
Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akimkabidhi Makamu Mwenyekiti wa taasisi
ya Hassan Maajar Trust Bw. Shariff Maajar shilingi laki moja na nusu ili
aikabidhi kwa mwalimu mkuu shule ya msingi Kasense ikiwa ni sehemu ya
azimio alilolianzisha na kuliita "Azimio la Kasense" KADARU (Kampeni ya
Dawati Rukwa) katika hafla fupi kukabidhi madawati 320 ya taasisi ya
Hassan Maajar Trust kwa shule za msingi Mkoani Rukwa tarehe 06-06-2013.
Makamu Mwenyekiti wa
taasisi ya Hassan Maajar Trust Bw. Shariff Maajar akizungumza katika
hafla fupi kukabidhi madawati 320 ya taasisi hiyo kwa shule za msingi
Mkoani Rukwa tarehe 06-06-2013 katika shule ya msingi Kasense, Kulia
kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya, Katibu Tawala
Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima, Meya Manispaa ya Sumbawanga
Sabas Katepa na Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Hassan Maajar
Trust Bi. Zena Tenga.
Mkuu wa Mkoa wa
Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akipima uelewa wa baadhi ya wanafunzi wa
shule ya msingi Kasense Mkoani Rukwa kwa kuwapa mtihani wa kuandika
wakati wa hafla fupi kukabidhi madawati 320 ya taasisi ya Hassan Maajar
Trust kwa shule za msingi Mkoani Rukwa tarehe 06-06-2013 katika shule
hiyo, Kulia ni Mstahiki Meya Manispaa ya Sumbawanga Sabas Katepa.
Kutoka kushoto ni
Makamu Mwenyekiti Hassan Maajar Trsut Bw. Shariff Maajar, Mkuu wa Mkoa
wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya, Mstahiki Meya Manispaa ya Sumbawanga
Sabas Katepa na Mkurugenzi Mtendaji Hassan Maajar Trust Bi. Zena Tenga
wakifurahia Ngonjera ya wanafunzi wa shule ya msingi Kasense katika
hafla hiyo ya kukabidhi madawati.
Picha ya pamoja
kati ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya, viongozi wa
Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga na viongozi wa taasisi ya Hasaan
Maajar Trust.
Picha ya pamoja.
(Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa)
0 comments:
Chapisha Maoni