Mkuu
wa Wilaya Songea Ndg. Joseph Joseph Mkirikiti akiwapa maelekezo wafanya
biashara ambao hufanya biashara zao kwa kupanga kandokando ya barabara
kuu kitendo ambacho ni kinyume cha sheria za usalama barabarani.
Baada
ya kupewa maelekezo na mkuu wa wilaya mama huyu ambaye hakufahamika
jina lake kwa kuwa ni mwelewa akaamua kukusanya bidhaa zake na kuelekea
maaneo waliyotengewa kufanyia biashara zao ambayo ni Majengo.
Mkuu
wa wilaya akiendelea kutoa somo kwa machinga ambao walikuwa upande wa
pili kuwa si sahihi kufanya biashara maeneo hayo kwani ni hatari hasa
kwa waendesha vyombo vya moto pamoja na watumiaji wengine wa barabara
ambao baadhi huwa hawako makini wawapo barabarani .
Baada
ya kutoa soma kwa waelewa na waungwana huwa wanatekeleza na kuondoka
kama inavoonekana hapa huyu mfanya biashara akielekea sehemu
waliyotengewa kufanya biashara maaeneo ya Majengo.
Mkuu
wa wilaya ya songea Ndg. Joseph Josep Mkirikiti akisalimiana na moja wa
vijana wake ambaye amekuwa akikimbizana naye mara kwa mara juu ya
kufanyia biashara kandokando ya barabara ikiwa ni pamoja na eneo la
Dilux, Soko kuu na kituo kikuu cha Mabasi mjini Songea.
Kijana
huyo ambaye hakufahamika jina mara moja alimueleza mkuu wa wilaya kuwa
hii sehemu huwa wanapenda kufanya biashara kwani ni sehemu ambayo ni ya
mchanganyiko wa watu wengi ambao huwa wanapita katika maeneo hayo pia
kwa wasafiri ambao huwa ndio wateja wao wakubwa.
Baada
ya mkuu wa wilaya kusalimiana na rafiki yake ambaye mara kwa mara
wamekuwa maeneo tofauti tofauti yasiyo ruhusiwa kufanyia biashara na
kijana huyo kumweleza tatizo lake aliamua kumpa fedha zimsaidie kujikimu
baada ya kumoona kijana huyu ni mchakalikaji wa kutafuta maisha.
Somo
linapokolea haina haja ya kutumia nguvu kama inavyoonekana katika picha
hiyo hapo juu , Kijana huyo akikusanya biashara yake kwa amani tayari
kuelekea katika sehemu husika amabyo wametengewa na serikali kwa ajili
ya kufanyia biashara zao.
Hata
hivo Mkuu wa wilaya ameendela kusema kuwa eneo wanalofanyia biashara
zao sio eneo salama kwani eneo hilo ni finyu nalinaweza kusababisha
ajali kwa watumiaji wa barabara.
Kwa
sababu baadhi yao wamekuwa wakipanga biadhaa zao bara barani na
kusababisha kuziba njia kama inavyoonekana katika picha hapo juu.
Aidha
Joseph Mkirikiti ametoa ushauri kwa wafanya biashara wadogowadogo
maarufu kwa jina la machinga kuwa na umoja kwa kuunda vikundi vyenye
uongozi ili kurahisisha mawasiliano yao na mamlaka zilizopo ikiwa ni
pamoja na ofisi ya manispaa ya Songea .
Pia
amewashauri wafanya biashara hao wadogowadogo kufikiria kupanua wigo wa
kufanyia biashara zao badala ya kunga’anga’nia kufanyia biashara hizo
katikati ya mji kwani eneo hilo ni finyu.
Habari na Picha kwa Hisani ya www.demashonews.blogspot.com
0 comments:
Chapisha Maoni