JULIO CESAR
Arsenal wapo mbioni kumsainisha
mkataba mnono mmoja kati ya magolikipa bora wa ligi kuu England wa klabu
ya Queens Park Rangers mbrazili Julio Cesar baada ya kumalizika kombe
la Confederations linaloendelea nchini Brazil ambapo fainali ni kati ya
Brazili na Hispania.
Arsene Wenger amesema anataka
golikipa mwenye uzoefu na ambaye ataleta ushindani na magolikipa wake wa
sasa Lukasz Fabianski na Wojciech Szczesny.
mazungumzo kati ya Arsenal na Cesar
tayari yameshafanyika ila bado makubaliano kutokana na mlinda mlango
huyo kuwa na majukumu na timu yake ya Taifa.
CESAR KATIKA MIKIKI MIKIKI YA KULINDA LANGO.
0 comments:
Chapisha Maoni