WAYNE ROONEY
Kocha mpya wa Manchester United David
Moyes amesema wiki ijayo atakaa meza moja na mshambuliaji nguli wa klabu
hiyo ambaye pia ashawahi kumfundisha akiwa Everton Wayne Rooney ili
kujaribu kumshawishi asiondoke klabuni hapo na kusahau tofauti zake na
kocha aliyestaafu Sir Allex Ferguson badala yake aelekeze juhudi zake
kuisaidia klabu kutetea ubingwa wao wa ligi kuu walioupata msimu
uliopita
Taarifa za ndani kutoka kwa marafiki wa ROONEY zinasema msimamo wake wa kuondoka klabuni hapo upo pale pale na malengo na shauku yake ni kutua CHELSEA kufanya kazi na kocha anayemzimia kwa muda mrefu Jose Mourinho
DAVID MOYES-KOCHA MPYA WA MAN U
Enzi hizo Rooney akiwa Everton na Moyes.
0 comments:
Chapisha Maoni