Wananchi
wa Tanzania wameelezwa kuwa kazi ya kuboresha huduma za afya na afya ya
mazingira na maji ni ngumu na kuwa inahitaji nguvu za pamoja kati ya
jamii, halimashauri na wadau mbalimbali ili kupata mafanikio
yaliyokusudiwa hasa ya uzuiaji wa magonjwa.
Akitoa
nasaha wakati wa kufunga wa zoezi la utoaji wa huduma za afya kwa
uwiano katika jamii kata ya Gombo la Mboto, Mgeni rasmi Mh. Jerry Silaa,
Mstahiki Meya wa halmashauri ya Manispaa ya Ilala amesema huduma za
afya na afya ya mazingira ni muhimu katika maisha ya kila siku ya
binadamu.
Ameongeza
kwa kuwapongeza sana wakazi wa Gomngo la mboto Markaz pamoja na
viongozi wao kwa juhudi kubwa walioifanya katika kuhakikisha uwepo wa
kituo cha tiba karibu na jamii na kuwa wanastahili kuwa mfano wa kuigwa
na jamii zingine.
Aidha
amesema hilo ni moja wapo katika utekelezaji wa agizo la Mh. Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika lengo lake la kupeleka huduma za
tiba zikiwamo zile za zinazohitaji madaktari bingwa karibu na wananchi.
Pichani
juu na chini ni wakazi wa Gongo la Mboto wakimsikiliza Diwani wao
ambaye pia ni Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa
wakati wa kufunga zoezi la utoaji wa Huduma za Afya kwa Uwiano katika
Jamii kata ya Gongo la Mboto.
Mganga
Mkuu wa Manispaa ya Ilala Dr. Asha Mahita akielezea dhamira ya Idara
katika kuendeleza Afya ya Jamii kwa kusogeza Huduma za Afya karibu na
Jamii, Huduma hizo zinahusisha matibabu kwa magonjwa mbalimbali kama
Magonjwa ya Moyo, Kisukari, Malaria, Macho, Meno, Afya ya Akili, Ushauri
na kupima VVU kwa hiari, Elimu juu ya Uzazi wa Mpango na Afya ya Uzazi,
Afya ya Mazingira, Lishe, na Jinsia, pia ametoa tathmini ya wakazi wa
Kata ya Gongo la Mboto Markaz waliopatiwa huduma za Afya bure kwa zoezi
lililofanyika kwa muda wa siku tatu ikiwemo Afya ya Akili, Kifua Kikuu
na matibabu ya Ujumla.
Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto ambaye pia ni Mstahiki Meya
wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akifurahia jambo na mmoja wa wakazi wa
kata ya Gongo la Mboto aliyefika katika Zahanati hiyo kupatiwa Huduma
ya Bure.
Diwani
wa Kata ya Gongo la Mboto, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry
Silaa akipima Presha wakati wa kufunga zoezi la Utoaji wa Huduma za Afya
kwa Uwiano katika jamii ikiwa ni ishara ya kuhamasisha watu kujenga
utamaduni wa kupima Afya zao.
Wakazi
wa Kata ya Gongo la Mboto wakipatiwa dawa za bure baada ya kufanyiwa
vipimo wakati wa kutoa Huduma ya Upimaji Afya Bure kwa wakazi wa kata
hiyo iliendehshwa kwa siku tatu.
Diwani
wa Kata ya Gongo la Mboto Jerry Silaa akifurahi jambo na watoto
waliofika katika Zahanati hiyo kupatiwa huduma ya Upimaji Afya bure.
Mtaalamu
wa Magonjwa ya Kisukari kutoka Kituo cha Afya Amana Dkt. Abushiri
Rajabu akitoa maelezo kwa Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto Jerry Silaa
kuhusu Elimu anayotoa kwa jamii kuhusiana na Ugonjwa huo.
0 comments:
Chapisha Maoni