Searching...
Jumatatu, 6 Mei 2013

RAIS WA ZANZIBAR ATUA PEMBA KUWASHA MWENGE WA UHURU.

 Rais wa  Zanzibar na  Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mh, Dk. Ali Mohamed Shein akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Jeshi na Usalama  wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Pemba Mei,5,2013 ,kwaajili ya uzinduzi  wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Chokocho wilaya ya Mkoani mkoa wa Kusini Pemba tarehe 6, Mei,2013.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Chakechake Mwanajuma Majid Abdalla katika kiwanja cha ndege  cha Pemba Mei,5.2013 tayari kwa uzinduzi wa  mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa hapo Mei 6,2013 katika  sheiha ya Chokocho, wilaya ya Mkoani mkoa wa Kusini Pemba.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mh, Balozi Seif Iddi (kulia) akisalimiana  na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mh, Dk. Fenella Mukangara (kushoto)  katika uwanja wa ndege Pemba,  Mei,5,2013 alipowasili kwaajili ya kuhudhuria uzinduzi wa mbio  za Mwenge  wa uhuru Kitaifa Mei,6,2013 katika  sheiha ya Chokocho wilaya ya Mkoani mkoa wa Kusini Pemba.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Mh.Balozi  Seif Iddi (kulia) akisalimiana na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar,Mh, Pandu Kificho katika uwanja wa ndege Pemba Mei,5,2013
Kikundi cha brass- band ya vijana  wakitumbuiza wakati wa mapokezi ya Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mh. Dkt. Ali Mohamed Shein(hayupo pichani) katika uwanja wa ndege wa Pemba ,Mei,5,2013.
Baadhi wa viongozi wa chama na serikali wakiwa katika uwanja wa ndege wa Pemba kumlaki Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar  Mh. Dkt.Ali Mohamed Shein(hayupo pichani),kwaajili ya uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Chokocho Wilaya ya Mkoani, mkoa wa Kusini Pemba, Mei 5,2013.
Picha  na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO.


0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!