KOCHA JOSE MOURINHO.
Kocha wa timu ya Real Madrid Jose
Mourinho amesema hatoendelea na kazi yake kama kocha wa Madrid msimu ujao na
badala yake amesema na badala yake amesema atakwenda mahali ambapo watu
wanataka awepo.
Baada ya mechi ya jumanne
aliyoshinda mabao mawili kwa sufuri dhidi ya borusia Dotmund japo hayakutosha kuwapeleka fainali Morinyo
alisema
"Najua napendwa sana England, Najua
napendwa na vilabu kadhaa pale England na zaidi ni klabu moja maalum"
Lakini akasisitiza kwamba atasubiri
kuchukua maamuzi hadi hapo msimu utakapomalizika"sijachukua maamuzi yoyote
kuhusu maisha yangu baada ya hapa mpaka sahivi kwasababu bado nina mkataba na
klabu na ninauheshimu mkataba wangu na na klabu pamoja na rais wa klabu,nataka
kukaa chini na rais nizungumze naye kuhusu uamuzi huu.
Mourinho aliiacha klabu ya Chelsea the Blues katika
hali tete mwezi September 2007, baada ya kushindwana na tajiri na mmiliki wa klabu
hiyo mrusi Roman Abramovich japo ameendelea kubaki katika historia ya klabu ya
timu hiyo kuwa kocha aliyeiletea vikombe vingi klabu hiyo.
Hata hivyo tetesi zimezidi kuzagaa
kwamba Mourinho anarejea Chelsea baada ya kocha wa sasa wa Chelsea Rafael
Benitez kusema kwamba ataondoka Chelsea mwishoni mwa msimu huu
“"Ninapendwa na mashabiki na vyombo
vya habari ambao wananitendea haki ,ninajua Hispania ni tofauti kwasababu watu
wengi wananichukia" Alisema Mourinho.
0 comments:
Chapisha Maoni