Pichani
ni baadhi ya waombolezaji waliokutwa na mtandao huu nyumbani kwa
marehemu Dk. Masau, Mbweni Kwajumbe, nje kidogo ya jiji la Dar es
salaam. Imeelezwa kuwa Dk. Masau anatarajiwa kuugwa kesho katika
Hospitali ya Aghakan saa 5:00 asubuhi. Baada ya hapo mwili utarudishwa
nyumbani kwake kabla ya kusafirishwa kesho kutwa kwenda kwa maziko
kijijini kwao Murutunguru, Wilaya ya Ukerewe.
baadhi ya waombolezaji wakiwa msibani nyumbani kwa marehemu mapema leo
Mjane wa marehemu, Janeth kazara Masau (kulia), akifarijiwa na majirani zake nyumbani kwake leo.
...waombolezaji msabani leo.
Dr. Ferdnand Masau, enzi za uhai wake
Taasisi ya Moyo ya Tanzania ya Dr Masau
Marehemu
Dk. Masau, ambaye alifariki dunia juzi May 16 majira ya asubuhi katika
Hospitali ya Aga khan alikokuwa amelazwa kwa siku kadhaa, ameacha mke na
watoto watano. Mungu alitoa na Mungu ametwaa, jina lake lihimidiwe.
Rest In Peace Dk..Ameen!
PICHA: Makongoro Oging/GPL
0 comments:
Chapisha Maoni