Searching...
Ijumaa, 3 Mei 2013

CHADEMA WATOA MSIMAMO MKALI KUHUSU HATMA YA RASIMU YA KATIBA MPYA

Akisoma hotuba ya kambi rasmi ya upinzani bungeni ya wizara ya katiba na sheria ambaye pia ndiye mnadhimu wa kambi hiyo bungeni mheshimiwa TUNDU LISU hapa amekaririwa akisema
 "Endapo hadi kufikia mwisho wa kipindi hicho Serikali itakuwa haijaleta Muswada wa marekebisho yanayotakiwa; au endapo Muswada utakaoletwa hautakidhi matakwa ya kuboresha mchakato wa upatikanaji wa Katiba Mpya, basi CHADEMA itawaalika wanachama, wafuasi na mashabiki wake Tanzania nzima, pamoja na taasisi za kiraia na za kidini, vyama vya siasa na Watanzania wote wenye nia njema na taifa hili kuhamasisha Watanzania kuikataa Rasimu ya Katiba Mpya kwenye kura ya maoni itakayofanyika kwa ajili ya kuihalalisha Katiba hiyo."-Tundu Lissu, Waziri Kivuli Katiba na Sheria.
                   Huu ndio msimamo wetu rasmi.

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!