HATIMAYE ULE MSEMO WA WAHENGA USEMAO "HAYAWI HAYAWI YAMEKUA" SASA UMETIMIA BAADA YA KOCHA MRENO MWENYE HISTORIA YA MAFANIKIO YA UFUNDISHAJI SOKA DUNIANI NA KIPENZI CHA WACHEZAJI NA MASHABIKI WENGI WA SOKA DUNIANI HASA WA CHELSEA JOSE MOURINHO "SPECIAL ONE" HATIMAYE AMEMALIZANA NA TAJIRI NA MMILIKI NA KLABU YA CHELSEA ROMAN ABRAHIMOVICH TAYARI KURUDI TENA DARAJANI STMFORD BRIGE KUKINOA KIKOSI HICHO ALICHOKINOA KWA MAFANIKIO MAKUBWA.
HABARI KUTOKA VYOMBO MBALIMBALI VYA HABARI ULAYA VINASEMA MRENO HUYO MWENYE MANENO
MENGI JANA USIKU AMEMALIZANA NA TAJIRI ABRAHAMOVICH KWENYE MGAHAWA WA LA FAMIGLIA MAGHARIBI MWA LONDON AMBAPO SASA MOURINHO ATAVUNA JUMLA YA PAUNDI MILIONI KUMI KWA MWAKA.
TAARIFA ZAIDI ZINASEMA ILI KUKAMILISHA DILI HILO SASA MOURINHO ATAPASWA KUWALIPA MADRID PAUNDI MILIONI 12 ILI KUVUNJA MKATA WAKE NA KLABU HIYO YA HISPANIA.
TAARIFA ZIMEZIDI KUELEZA KWAMBA MOURINHO AMESHAPEWA RUNGU LA KUANGALIA WACHEZAJI ATAKAOWASAJILI NA WALE ATAKAOWATEMA KATIKA KIKOSI CHA SASA AMBAPO INASEMEKANA WACHEZAJI KADHAA KUTOKA MADRID,BARCELONA,BORRUSIA DOTMUND,BARYEN MUNICH NA ATLETICO MADRID WATATUA DARAJANI NA MRENO HUYO ANAYETARAJIWA KUTUA RASMI CHELSEA JULAI MOSI MWAKA HUU.
0 comments:
Chapisha Maoni