Searching...
Jumanne, 30 Aprili 2013

UHOLANZI YAPATA MFALME MPYA.

  Mfalme mpya wa Uholanzi Willem Alexander
 Mfalme Willem Alexander kushoto,katikati mama yake aliyemkabidhi madaraka na pembeni ni mke wa mfalme.
Malkia Beatrix wa Uholanzi amesaini kanuni ya kumpa kiti mwanawe Willem Alexander, Mfalme wa kwanza wa nchi hiyo kwa zaidi ya miaka 100. Umati wa Watu ulimiminika asubuhi ya leo mjini Amsterdam kushuhudia sherehe hiyo.
Malkia Beatrix , mwenye haiba ya kupendwa na wengi amemaliza utawala wake wa miaka 33 leo, katika sherehe iliyotangazwa moja kwa moja na Televisheni na utiaji saini wa kumkabidhi Ufalme mwanawe wa kiume kushuhudiwa na maelfu ya Waholanzi waliovalia sare za rangi ya machungwa. Pia sherehe hiyo imeshuhudiwa na mamilioni ya watazamaji kwa njia ya Televisheni.
Kutokana na kuuacha Umalkia, Beatrix sasa anakuwa Princess Beatrix na mwanawe anakuwa Mfalme Willem Alexander, mfalme wa kwanza wa Uholanzi tangu alipofariki Willem wa tatu 1890.
Mfalme Willem-Alexander mwenye umri wa miaka 46, mkewe mzaliwa wa Argentina Malkia Maxima na watoto wao watatu wakike walihudhuria sherehe hiyo ya leo. Binti yao wa kwanza Catharina-Amalia mwenye umri wa miaka 9 ndiye mrithi wa kwanza wa kiti baada ya baba yake. Wengine ni Alexia mwenye umri wa miaka 7 na Ariane miaka 5.
 Mfalme Willem Alexander na familia yake
Mfalme Willem Alexander na familia yake.

Ilikuwa shamra shamra kwa wakazi wa Amsterdam
Waholanzi wakishangilia kumpata mfalme mpya.
 habari na picha kwa msaada wa DW-Swahili.
 

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!