Searching...
Jumanne, 30 Aprili 2013

LEO NDIO LEO KLABU BINGWA ULAYA.JE MADRID ATALIPA KISASIII???

Real Madrid vs Borussia DortmundBaada ya vijana wa Mourinyo wakiongozwa na mreno Christian Ronaldo kukubali kipigo cha mabao manne kwa moja kutoka kwa Borusia Dortmund wiki iliyopita katika nusu fainali ya kwanza iliyopigwa nchini ujerumani,hatimaye leo wajerumani hao wametua nchini Hispania kumalizia ngwe hiyo ya nusu fainali ya pili.
wengi wa watabiri wa soka duniani wamesikika wakisema Madrid hana lake tena baada ya kipigo hicho lakini Mourinyo na timu yake ya wapiganaji wamewatoa hofu mashabiki wake kwamba lazima watashinda kwa kishindi na kutinga nusu fainali kule WIMBLEY .... kesho ni zamu ya Barcelona na wajerumani wengine Baryen Munich,ambapo Barca nao wanatarajia miujiza kuingia fainali baada ya kukubali kipigo cha mabao manne kwa sufuri kule nchini ujerumani wiki iliyopita.
hakuna ajuaye kipi kitatokea zaidi ya kusubiri dakika tisini kuanzia saa nne na dakika arobaini na tano usiku wa leo kama Mourinyo atafanya alichosema au ataongezewa tena kapu la magoli. 
 
Matokeo wiki iliyopita katika nusu fainali ya kwanza.

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!