Searching...
Alhamisi, 19 Oktoba 2017

KOCHA WA LEICESTER CITY AFUKUZWA KAZI.


CRAIG SHAKESPEARE-KOCHA WA LEICECTER CITY ALIYEFUTWA KAZI.
LONDON: Klabu ya soka ya Leicester City inayoshiriki Ligi Kuu ya England imemfuta kazi kocha wao Craig Shakespeare ikiwa ni miezi minne tu baada ya kusaini kandarasi ya miaka mitatu akichukua nafasi iliyoachwa wazi na bosi wake Claudio Ranieri ambaye alifukuzwa mapema msimu uliopita baada ya mabingwa hao wa mwaka 2016-2017 kuanza vibaya.

The Foxes kama wanavyojiita wako nafasi ya tatu kutoka chini katika jedwali la ligi ya Uingereza na hawajashinda mechi yoyote miongoni mwa mechi sita walizocheza.
Shakespeare alishinda mechi 8 kati 16 akiwa mkufunzi wa timu hiyo msimu uliopita na kuisaidia klabu hiyo kufika katika robo fainali ya kombe la vilabu bingwa Ulaya.
Shakespeare amefutwa kazi baada ya timu hiyo kupata sare ya 1-1 dhidi ya West Brom siku ya Jumatatau wiki hii.
CLAUDIO RANIERI-KOCHA MTANGULIZI WA SHAKESPEARE.
Mara ya mwisho kwa Leicester kucheza mechi sita bila ushindi Claudio Ranieri alifutwa kazi , miezi tisa baada ya kuisaidia timu hiyo kushinda taji la ligi.

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!