MHE. PETER MSIGWA AKIWASILI VIWANJA VYA MAHAKAMA IRINGA.
IRINGA: Taarifa kutoka Mkoani Iringa zinasema Mbunge wa Iringa Mjini Mhe. Mchungaji Peter Msigwa amefikishwa Mahakamani kwa madai ya kumtusi na kutishia kumuua aliyekuwa Diwani wa Kata ya Kitwiru, Baraka Kimata.
Mbali na Mchungaji Msigwa, pia Diwani wa Viti Maalum Mhe.Selestina Johanes na dereva wa mbunge huyo Bw. Godi Mwaluka nao pia wamepandishwa kizimbani kwa kosa hilo.
akisoma shitaka hilo Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Mhe. Rehema Mayagilo amesema kuwa mbunge huyo pamoja na washitakiwa hao wawiliwanatakiwa kujibu tuhuma za kumtishia kumuua diwani huyo.
Hata hivyo mara baada ya kusomewa shitaka hilo watuhumiwa wote wamepatiwa dhamana na kesi hiyo imeahirishwa hadi Octoba 09 mwaka huu itakapotajwa tena.
0 comments:
Chapisha Maoni