Searching...
Jumapili, 6 Julai 2014

PAUNDI MILIONI 45 + LUIS NANI =ARTURO VIDAL MAN UTD

LOUIS VAN GAAL.
Mipango kabambe ya kocha wa Manchester United mholanzi Louis Van Gaal kukiimarisha kikosi hicho msimu ujao inazidi kupamba moto hadi kuwafanya wapenzi wa soka kuona huo mseto wa kikosi chake msimu ujao kutokana na usajili wake wa kila kukicha.
 manchester united, mufc, man united, david moyes, moyes, old trafford, louis van gaal, van gaal, arturo vidal, vidal, nani, arsenal, arsenal fc,
ARTURO VIDAL.
Sasa Van Gaal anamtaka kiungo mkabaji wa Juventus Arturo Vidal kwa gharama yoyote ile,ambapo kwa mwanya huo Juve wametoa masharti makubwa ambapo sasa wamesema hawana shida kumuachia kiungo wao huyo lakini lazima Man U watoe paundi milioni 45 sambamba na mchezaji wao mshambuliji wa pembeni Luis Nani vinginevyo mpango huo hauwezi kukamilika,masharti ambayo kwa hakika yanampasua kichwa sana Van Gaal.

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!