Searching...
Jumapili, 6 Julai 2014

WENGER AANZA KAZI,ALAMBA DUME BEKI NEWCASTLE,LIVERPOOL HOIIII



ARSENE WENGER.
Hatimaye vita ya kumuwania Beki kisiki na tegemeo la Newcastle United Mathieu Debuchy mwenye umri wa miaka 28 ambaye alikua anagombewa na timu mbalimbali ulaya ambapo mwisho wa siku zilisalia Liverpool na Arsenal,hatimaye babu mbahili Arsene Wenger amelamba dume baada ya mchezaji mwenyewe kuwaambia wanahabari jana jumamosi kwamba yeye anahamia Arsenal na sio Liverpool. 
 
MATHIEU DEBUCHY.
Mathieu Debuchy anakwenda Arsenal akijua fika kwamba anakwenda kuchukua namba ya Bacary Sagna ambaye ametimkia Manchester City,na taarifa zinasema Debuchy atasaini mkataba wa miaka minne na klabu hiyo kwa gharama ya paundi milioni 12.

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!