Searching...
Jumapili, 6 Julai 2014

NI WENGER TENA,AZIVURUGA MAN U NA LIVERPOOL-NYOTA WA CHILE KUTUA MUDA WOWOTE

ARSENE WENGER.
Taarifa za kusikitisha kwa upande wa Liverpool lakini wa furaha na shangwe kwa klabu ya Arsenal ni kwamba muda wowote kuanzia sasa ndani ya saa 24 mchezaji wa timu ya taifa ya Chile aliyekua akikipiga na klabu ya Barcelona Alex Sanchez atatua rasmi Emirates baada ya kufikiwa kwa makubaliano kati ya Barcelona na Arsenal ambapo sasa Wenger kocha Mfaransa anayesifika kwa sifa ya ubahili itamlazimu kuvunja Benk na kutoa kitita cha paundi milioni 32 ili Mchile huyo aliyeonyesha cheche kwenye kombe la dunia aweze kutua Arsenal.
  ALEX SANCHEZ.
Barcelona wanalazimika kumtoa mchezaji huyo sio kwamba hana kiwango bali ni kwaajili ya kupata pesa za kumnunua mchezaji mla watu na mnyonyaji wa damu za wachezaji wenzake Luis Suarez ambaye kwa sasa mazungumzo kati ya Barcelona na Liverpool yanaendelea vizuri na huenda Suarez akatua Barcelona mapema wiki ijayo.
BANNER ArsLiv4.jpg
Sanchez, amekua akiwindwa na vilabu mbalimbali barani uropa baada ya kufanya vizuri huko Brazili ambapo Liverpool,Arsenal na Manchester United,lakini kwa taarifa hizi sasa ni dhahiri kwamba itakua ni hitimisho la uvumi huo.

0 comments:

Chapisha Maoni

:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Back to top!