Mchezaji bora wa tenesi duniani amejikuta katika wakati mgumu katika mashindano ya Wimbledon baada ya kucharazwa na kutupwa nje ya michuano na kijana mdogo anayechipukia katika mchezo huo kutoka nchini Australia Nick Kyrgio. 
  

  
Mchezaji kinda wa mchezo wa Tennesi Nick Kyrgios akishangilia ushindi baada ya kumgalagaza mkongwe Rafael Nadal katika mashindano ya Wimbledon. 
 
 
 
  

  
Mchezaji huyo kinda wa Australia Nick Kyrgios amesema hajui aseme nini baada ya ushindi huo mkubwa na ndoto katika maisha yake. 
 
 
 
  

  
Nimekubali yaishe-mkongwe Nadal akimpongeza kinda baada ya ushindi wa ajabu kwa mchezaji huyo kijana. 
 
 
 
  

  

 Rafael Nadal alijitahidi kwa nguvu zake zote lakini alikwaa kisiki kwa kijana Nick Kyrgios kutoka nchini Australia.
 
 
 
 
 
  

  
Mashabiki wa kijana Nick Kyrgios walicharuka baada ya kumng'oa Nadali katika mashindano hayo ya Wimbledon. 
 
 
 
 
0 comments:
Chapisha Maoni