Nahodha wa timu ya taifa ya Uholanzi na tegemeo kubwa la timu hiyo na klabu yake ya Manchester United Robin van Persie (kushoto) ameumia vibaya mazoezini na kuondolewa kunako kambi ya timu hiyo huko Rio nchini Brazili na kuzua hofu kubwa kwa wapenzi na mashabiki wa timu ya Uholanzi na Man U.
Taarifa zinasema mchezaji huyo alitolewa uwanjani akiwa amefungwa bandeji lakini daktari wa timu hiyo hakuweza kufafanua mara moja kwamba ameumia wapi na kiasi gani na kama atashindwa kucheza robo fainali au lah.
Endapo tegemeo hilo la Uholanzi atashindwa kushuka dimbani kuwavaa Costa Rica kunako mtanange wa robo fainali basi Klaas-Jan Huntelaar anatarajiwa kuchukua nafasi yake.
Timu ya taifa ya Uholanzi wakijadili jambo wakati wa mazoezi kabla ya kuwavaa wa Costa Rica
Mshambuliaji wa Pembeni wa Uholanzi Arjen Robben (mbele) yeye yupo fiti kuwavaa wacosta Rica ili kutafuta tiketi ya kucheza nusu fainali ya michuano hiyo.

0 comments:
Chapisha Maoni