HUYU NDIYE KIJANA ANAYEZUNGUKA BARA LA AFRIKA KWA BAISKELI.
Home
»
Unlabelled
» HUYU NDIYE KIJANA ANAYEZUNGUKA BARA LA AFRIKA KWA BAISKELI.
Derek Cullen
ni kijana wa miaka 32 aliki kwa sasa hana mama wala baba baada ya kufiwa na wazazi wake wote wawili kwa ugojwa wa Kansa na sasa anazunguka bara zima la Afrika kwaajili ya kuchangisha pesa kwaajili ya kuanzisha kituo cha kutibu ugonjwa huo bure.
safari ya Derek Cullen itampitisha katika nchi saba barani Afika ambapo alianzia huko jijini Cape Town nchini Afrika Kusini na sasa tayari ameshapita Botswana,Tanzania na Kenya.
Derek Cullen wakati anaianza safari yake mwezi wa kumi na moja mwaka jana nchini Afrika Kusini.
Derek akiwa amepozi na baiskeli yake kabla ya kuianza safari.
Derek akiianza safari yake ya kuchangisha pesa kwaajili ya kuanzisha Charity ya ugonjwa wa kansa.
Derek anapita sehemu mbalimbali zenye kila aina ya wanyama na wadudu hatari kama hapo akipishana na kinyonga barabarani.
Pamoja na kikwazo cha lugha lakini Derek amekua akipita katika vijiji mbalimbali na kukutana na watu wa nchi na vijiji vyenye makabila na kuongea lugha tofauti tofauti lakini kwake sio kikwazo kwani amekua akuwasiliana nao hata kwa ishara.
Derek akiulizia wapita njia maswali kadhaa ikiwa ni pamoja na sehemu ya kupata mahitaji muhimu.
Derek akiwa amejipumzisha kwenye kivuli na baiskeli yake kabla ya kuendelea na safari yake ya kulizunguka bara la Afrika kwa Baiskeli.
Hapa Derek akiwa amejipumzisha kwenye hema lake.
Derek akiwa na koti lake la mvua akikatisha mbuga kuelekea nchini Namibia huku watoto wakimshangaa.
Derek anasema wakati wa mvua anajisikia nguvu zaidi na anaweza akaendesha baiskeli yake kwa muda mrefu zaidi kuliko wakati wa jua.
Sehemu nyingine hali inakua ya joto sana na ilibidi Derek ajimwagie maji ili aweze kuendelea na safari yake.
Wakati mwingine kichwa kinauma ila safari lazima iendelee.
Derek akikatisha kati kati ya mbuga ya wanyama ya Mikumi huku akikutana na vibao vya tahadhari ya kuwepo kwa wanyama wakali.
hapa akikutana kwa karibu kabisa na tembo katika moja ya mbuga za wanyama nchini Botswana.
Akiwa katika moja ya kituo cha mafuta nchini Tanzania lakini anakuta kikiwa kimefungwa lakini baiskeli yake inatumia gesi kwahiyo haikua na shida.
Derek ni mcheshi sana na mpenda watu na kila mahali anapokutana na watu hupenda kuongea nao mambo mbalimbali.
Hapa bwana Derek akiwa nchini Kenya eneo la equator.
0 comments:
Chapisha Maoni