JOSE MOURINHO
Kocha wa Chelsea Mreno Jose Mourinho amefanya umafia baada ya kuingilia kati uhamisho wa mchezaji kiungo mshambulaji wa Bayern Munich Toni Kross kwenda Real Madrid baada ya jana jana usiku kupeleka ofa nono ya zaidi ya paundi milioni 25 zilizoahidiwa na Madrid,kitita ambacho kinailazimu Bayern Munich kuvunja mazungumzo na Real Madrid na taarifa zinasema uhamisho huo unaweza ukakamilika ndani ya saa 48 zijazo.
TONI KROSS
Bayern Munich wanalazimika kumuuza kiungo huyo huku bado udenda ukiwatoka kufuatia mchezaji huyo kugoma kuongeza mkataba na Bayern Munich msimu huu;japo aliombwa asaini na ataongezewa mshahara lakini bado akagoma.
0 comments:
Chapisha Maoni