MFUNGAJI BORA KOMBE LA DUNIA ATUPWA NJE,ALIA MACHOZI.
Home
»
Unlabelled
» MFUNGAJI BORA KOMBE LA DUNIA ATUPWA NJE,ALIA MACHOZI.
Mfungaji bora wa michuano ya kombe la dunia huko nchini Brazili Mkolombia James Rodriguez ameyaaga mashindano hayo baada ya kutolewa kwa timu yake na Brazili huku akiondoka na magoli 6 kibindoni baada ya jana kufunga goli zuri la penalti.
Mchezaji kinda na mfungaji bora James Rodriguez hatutomuona tena kombe la dunia baada ya Columbia kufungashiwa virago na Brazili.
James Rodriguez akishangilia goli lake la penalti dhidi ya Brazili jana japo walitupwa nje ya michuano kwa 2-1
Nahodha wa Brazili Thiago Silva akishangilia goli aliloifungia Brazili dakika ya 12 yas mchezo ila ataikosa mechi ya nusu fainali dhidi ya Ujerumani baada ya kupewa kadi mbili za njano.
Beki wa Brazili David Luiz akimpa pole James Rodriguez baada ya filimbi ya mwisho na Columbia kutolewa nje ya michuano na kuwaacha Brazili wakitinga nusu fainali.
Kocha wa Columbia Jose Pekerman akimfariji James Rodriguez baada ya dakika 90 kumalizika na kung'olewa mashindanoni.
Mungu akitupa uhai tutamuona Rodriguez kwenye kombe la dunia 2018 nchini Urusi kama Columbia watafuzu.
0 comments:
Chapisha Maoni