James Rodriguez akiondoka viwanja vya hospital ya Sanitas La Moraleja Madrid baada ya vipimo vyake kukamilika.
James Rodriguez alitarajiwa kutambulishwa rasmi leo jumanne katika uwanja wa Bernabeu mbele ya mashabiki wa Real Madrid.
James Rodriguez anatarajiwa kuleta chachu kubwa ya ushambuliaji katika kikosi cha Real ambapo ataungana na Ronaldo,Bale na Benzema.
Tayari nyota wa Ujerumani Toni Kroos alishasajiliwa mapema mwezi huu na kuifanya klabu hiyo ya Hispania kujaza nyota wengi wa soka Duniani...Swali ni Je,wataweza kupambana na miamba mingine ya Hispania kama vile Barcelona na Atletico Madrid?
0 comments:
Chapisha Maoni