Kiungo wa klabu ya Juventus na timu ya taifa ya Chile Arturo Vidal ameweka wazi kwamba yupo kwenye mazungumzo na klabu ya Manchester United ili kujiunga na mchezaji mwenzake Ander Herrera kunako dimba la Old Trafford?
Mchezaji huyo Arturo Vidal anaonekana wazi kutimkia Manchester
United, baada ya miamba hiyo ya soka ya England ambayo msimu uliopita waliweweseka na kuishia nafasi ya saba baada ya ligi kuisha na kumtimua kocha wao David Moyes sasa wanaonekana kusajili kwa nguvu chini ya kocha mpya Louis Van Gaal ambapo inasemekana wametuma ofa ya paundi milioni 40 ili kumng'oa kiungo huyo huko Juventus.
ARSENE WENGER.
Wakati mashetani hao wekundu wakisajili kwa kasi ya kimbunga nyikani,mashabiki wa Arsenal wamemlalamikia kocha wao Arsene Wenger kwa jinsi ambavyo haonekani kufanya usajili wa Ushindani kama wafanyavyo kocha wa Man U,Chelsea na Liverpool kitendo ambacho wanahofia kufanya vibaya msimu ujao.
0 comments:
Chapisha Maoni