Michuano ya kuwania ubingwa ama ufalme wa soka duniani umeendelea usiku huu huko nchini Brazili ambapo miamba miwili ya soka Argentina walishuka dimbani kusaka tiketi ya kucheza nusu fainali mtanange ambao umeitupa nje Ubelgiji kwa kichapo cha 1-0 kutoka kwa Argentina.

Goli pekee la Argentina lilifungwa na Gonzalo Higuain kufuatia pasi iliyokua haijalengwa kumuendea Higuan kugongwa kwa bahati mbaya na mchezaji wa Ubelgiji na kisha Higuan kuunganisha mpira huo kimiani na kumuacha mlinda mlango wa Chelsea akishuhudia mpira wavuni

Wachezaji wa Argentina wakishangilia ushindi

raha ya ushindiiiii

Nahodha wa timu ya taifa ya Ubelgiji Vincent Kompany akiwa hoi baada ya mpira kuisha na kuondolewa katika michuanol.

Mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi akifanya yake uwanjani japo bado ameendelea kukumbwa na ukame wa magoli katika michuano hii.
0 comments:
Chapisha Maoni
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.