JAMES RODRIGUEZ.
Moto na kasi ya klabu ya Manchester United kusajili unazidi kuwaka mithili ya moto wa petrol baada ya leo hii kutangaza dau nono kwa mfungaji bora wa kombe la dunia hadi sasa wa timu ya taifa Columbia James Rodriguez, baada ya kutuma ofa nono ya paundi milioni 65 kuinasa saini ya mchezaji huyo mtaalamu wa kuzifumania nyavu.Hadi kufikia jana ambapo Columbia ilifungwa na Brazili kwa shida,kinda huyo mwenye umri wa miaka 22 ambaye anakipiga pia na klabu ya Monaco alikua tayari kazifumania nyavu mara sita na kuongoza katika orodha ya wafungaji bora kombe la dunia nchini Brazili.
JOSE MOURINHO.
Hata hivyo haitakua rahisi kwa Man U kumnasa mchezaji huyo kufuatia taarifa kwamba vigogo wengine wa soka duniani Barcelona,Mardid na Chelsea wanammendea kinda huyo na tayari maofisa wa Chelsea wanaelezwa kutua Ufaransa kuzungumza na maofisa wa Monaco juu ya kumsajili nyota huyo huku wakitoa ofa ya paundi milioni 80.
LOUIS VAN GAAL.
lakini uwepo wa kocha wa Man U kwenye michuano ya kombe la dunia inasemekena kuwa ndio nguzo kubwa ya Man U kufanikiwa kuwanasa wachezaji mbalimbali kwani anatumia muda mwingi kutazama wachezaji bora wa mashindano na kuwaagiza maofisa wa Man u kufanya nao mazungumzo haraka.
0 comments:
Chapisha Maoni