TIMU YA TAIFA YA BRAZILI-2014
Baada ya mapumziko ya siku moja ya michuano ya kombe la dunia huko nchini Brazili,leo hii majira ya saa moja kamili usiku kwa saa za Afrika Mashariki michuano hiyo itaendelea kwa kuzikutanisha miamba ya soka duniani na wenyeji wa michuano hiyo mwaka huu Brazili dhidi ya miamba mingine ya soka kutoka huko Amerika ya Kusini Chile.
TIMU YA TAIFA YA CHILE-2014
Mechi hiyo itakayoamua nani wa kutinga robo fainali ya michuano hiyo mkubwa duniani itachezeshwa na mwamuzi wa kati polisi Howard Webb, mwamuzi msaidizi namba moja ni Michael Mullarkey,mwamuzi msaidizi namba mbili ni Darren Cann wote kutoka Uingereza na mwamuzi wa mezani ni Felix Brych kutoka nchini Ujerumani.
UWANJA WA ESTADIO MINEIRAO.
Mechi hiyo itachezwa katika uwanja wa Estadio Mineirao ambao una uwezo wa kuchukua watazamaji 58170 kwa wakati mmoja na kila mmoja akiwa amekaa kwente kiti chake, na uwanja huo umejengwa mwaka 1965.
0 comments:
Chapisha Maoni