RIO FERDINAND
Beki kisiki wa zamani wa Manchester United Rio Ferdinand ameishauri timu yake kipenzi ya Man U kuhakikisha hawapotezi muda kuinasa saini ya mchezaji wa Real Madrid Raphael Varane ambaye pia anawaniwa vikali na Chelsea.
RAPHAEL VARANE
Raphael Varane amekua akitolewa macho na vilabu vingi barani ulaya baada ya kufanya vizuri msimu uliopita na sahivi akiwa katika michuano ya kombe la dunia kule nchini Brazili pia amekua akifanya vizuri.
JOSE MOURINHO.
Lakini Man U watakumbana na ushindani mkubwa kutoka kwa Chelsea ambao kupitia kwa Mourinho ambaye alikua naye wakati akiwa kocha Madrid anamuwania kinda huyo kwa udi na uvumba na Varane anajua kwamba yeye ni kipenzi kikubwa cha Mourinho.
0 comments:
Chapisha Maoni