Home
»
Unlabelled
» VAN GAAL KUWAPORA LIVERPOOL MCHEZAJI WAO MKONGWE
Kocha wa timu ya taifa ya Uholanzi Louis Van Gaal ambaye anamalizia muda wake kabla ya kutimkia Man U baada ya tu ya kombe la dunia ameweka wazi kwamba anafanya kila liwezekanalo ili kumnasa mkongwe wa Liverpool Dirk Kuyt.
Dick Kuyt akiteta jambo na mshambuliaji wa United Robin van Persie katika mazoezi ya timu ya taifa huko nchini Brazili,ambaye kama usajili wake utakamilika basi watakua wote ndani ya uwanja wa nyumbani wa Old Trafford
Dick Kuyt ameitumikia klabu yake ya Liverpool kwa kipindi cha miaka sita na sasa Van Gaal anataka kutumia nafasi yake ya ukocha wa timu ya taifa kumshawishi kujiunga naye msimu ujao.
Dick Kuyte ni mmoja wa wachezaji wa timu ya taifa ya Uholanzi aliyeisaidia kuwafunga Hispania, Chile na Australia na kuondoka na pointi zote tisa za raundi ya kwanza katika michuano ya kombe la dunia inayoendelea huko nchini Brazili.
0 comments:
Chapisha Maoni