Zikiwa zimesalia saa chache kabla ya muendelezo wa michuano ya kulisaka kombe la dunia 2014 huko nchini Brazili,michuano ambayo ilikua imesimama kwa mapumziko ya siku moja, leo hatua ya 16 bora kutafuta tiketi ya robo fainali inaanza kwa wenyeji Brazili kuvaana na Chile mchezo ambao unatajwa kuwa mchezo mgumu kama wa fainali, lakini Chile tayari wamesema hawana imani ya mwamuzi wa mechi hiyo Howard Webb pichani juu.
Mchezaji wa Chile na klabu ya Barcelona Alexis Sanchez ndiye amekua wa kwanza kumshutumu mwamuzi huyo bora wa FIFA kwamba amekua na historia ya kupendelea timu fulani fulani kutokana na mapenzi yake kama vile shutuma mbalimbali za kuibeba Manchester United na inasemekana Webb ni mpenzi mkubwa wa timu ya taifa ya Brazil.
Shutuma za Chile zinakua na nguvu hasa pale wataalamu wa soka wanapoizungumzia penalti ya utata waliyopewa Brazil dhidi ya Croatia baada ya mchezaji wa Brazili Fred kujidondosha eneo la hatari.
0 comments:
Chapisha Maoni