BRENDAN RODGERS.
Hatimaye juhudi za wachezaji katika michuano ya kombe la dunia zinaanza kuzaa matunda baada ya Kocha wa Liverpool na kocha wa Man U Kuanza kampeni ya kuinasa saini ya mshambuliaji kinda wa Ghana aliyekua akikipiga nchini ufaransa na klabu ya Marseille Andrew Ayew ili kutua England kukipiga ligi kuu England.
ANDREW AYEW.
Mshambuliaji huyo kinda ameanza kuwaniwa na vilabu mbalimbali barani ulaya baada ya kuonyesha juhudi kubwa katika mechi kati ya Ghana na Ujerumani ambapo alikua nguzo imara iliyopelekea kutoka sare japo wametolewa kwenye michuano hiyo.
Andre Ayew kwa sasa hana mkataba na klabu yake ya Marseille kitendo ambacho kinaweza kikazirahisishia timu za ulaya kumnasa kiulani zaidi.
0 comments:
Chapisha Maoni