Wapenzi wa muziki wa Soul duniani wamekubwa na majozni makubwa baada ya legendari wa muziki huo duniani Bobby Womack kufariki dunia siku ya alhamisi tarehe 26-06-2014 akiwa na umri wa miaka 70.
Legendari huyo ametunga na kuimba nyimbo nyingi za kuvutia hisia za watu na kuwa kipenzi kikubwa cha wapenzi wa musiki duniani, lakini kwa hakika kwa sasa hatupo naye tena duniani baada ya kufariki wa ugonjwa wa Kansa.
Katika hali ya kuhuzunisha zaidi, ni wiki mbili tu zilizopita legendari huyo alifanya tamasha kubwa huko lililofahamika kama Bonnaroo Music Festival katika majiji ya Manchester na Tennessee nchini Uingereza.
Marehemu Bobby Womack alizaliwa huko Cleveland, Ohio. Na picha hii Bobby aliipiga mwaka 1964 akiwa na miaka 10.
Bobby Wommack enzi za uhai wake akiwa na wanamuziki wenzake mwaka 1970, baada ya kurekodi wimbo wake wa kwanza wa It's All Over Now uliotikisa dunia enzi hizo.
Hapa Bobby alikua akitumbuiza huko nchini Uholanzi mwaka 1976
0 comments:
Chapisha Maoni