Kocha mreno na mbwatukaji Jose Mourinho ameibwatukia FIFA kutokana na mpangilio mbovu wa mechi pamoja na viwanja vibovu huko nchini Brazil ambapo amedai kuwa zipo timu zinacheza ndani ya saa 24 jambo ambalo halikubaliki katika soka duniani.
Mourinho amesema haiingii akilini na haoni kama ni sawa Ureno na Marekani kucheza ndani ya saa 24 kabla ya Ujerumani na Ghana.
Mourinho ameenda mbali zaidi na kudai kuwa Ujerumani nao walicheza ndani ya saa 24 kabla ya Marekani 24 kabla ya Marekani ambao watawavaa katika mechi ya mwisho ya kundi G siku ya Alhamisi.
Sina raha na kombe la dunia msimu huu kutokana na mipango mibovu pamoja na viwanja vibovu vinavyosababisa wachezaji wazuri na timu nzuri kuonekana wabovu.
Hiki ni moja ya kiwanja anachokilalamikia Mourinho
0 comments:
Chapisha Maoni