Timu ya taifa yaAlgeria imetinga hatua ya 16 bora baada ya kutoka sare ya 1-1 na timu ya taifa ya Urusi na hivyo sasa bara la Afrika linawakilishwa na timu mbili za Aljeria na Nigeria.
Mchezaji wa Algeria Islam Slimani akifunga goli la kusawazisha dhidi ya Urusi na kuwawezesha kutinga 16 bora ya michuano ya kombe la dunia huko nchini Brazili.
Katika hatua ya 16 bora Algeria watacheza na Ujerumani huku Nigeria watakutana na Ufaransa siku ya jumatatu
Mashabiki wa Aljeria wakishangilia kwa mafataki baada ya mechi kuisha na kujihakikishia nafasi ya kusonga mbele hatua ya 16 bora.
0 comments:
Chapisha Maoni