Wahenga walisema kawia lakini ufike,hivi ndivyo yalipotimia pale Mkenya anayeichezea timu ya Ubelgiji alipoifungia timu hiyo goli la jioni mnamo dakika ya 88 mchezo dhidi ya Russia katika mechi iliyokuwa kali na ya kusisimua.
Mkenya Origi akitupia kambani mpira wa pasi nzuri kutoka kwa mchezaji nguli Eden Hazard na kuiwezesha Ubelgiji kutinga hatua ya 16 bora.
Nahodha wa Ubelgiji Vincent Kompany akishangilia goli la mkenya Origi baada ya kipenga cha mwisho ambacho kiliwahakikishia kutinga kumi na sita bora.
Eden Hazard akimshukuru Orig kwa kazi nzuri aliyoifanya katika mtanange huo uliochezewa katika uwanja wa Maracana.
Mchezaji wa Ubelgiji Thomas Vermaelen akitibiwa baada ya kupata majeraha katika mechi hiyo.
Baada ya maumivu kuzidi hapa Thomas Vermaelen analazimika kutoka na kumpisha Jan Vertonghen
Soka sio mchezo jamani,ni kama vita
mlinda mlango wa Urusi Igor Akinfeev akipangua mpira wa kichwa ulioelekezwa kwake na Marouane Fellaini
Kocha wa Urusi Fabio Capello akiwa haamini macho yake baada ya Mkenya kuiua Urusi dakika mbili kabla ya kipienga kupulizwa.
Mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku akijaribu kutumbukiza mpira kimiani pasipo mafanikio
Mchezaji wa Urusi Denis Glushakov akizawadiwa kadi ya manjano baada ya kumchezea ndivyo sivyo mchezaji wa Ubelgiji Dries Mertens.
Mlinda mlango wa Ubelgiji Thibaut Courtois gakipangua shuti kali kutoka kwa mshambuliaji wa Urusi.
Mshike mshike dimbani.
Kiungo mshambuliaji wa Ubelgiji Eden Hazard akijaribu kumtoka beki wa Urusi Denis Glushakov katika mpambano hu.
0 comments:
Chapisha Maoni