WANANCHI wa Afghanistan wamejitokeza kwa wingi jana Jumamosi (Aprili
5, 2014) kumchagua mtu wa kuchukuwa nafasi ya Rais Hamid Karzai katika
makabidhiano ya kwanza ya madaraka kwa njia ya kidemokrasia wakati
vikosi vinavyoongozwa na Marekani vikikamilisha vita yao vya miaka 13
nchini humo.
Licha ya vitisho vya kundi hatari la Taliban, upigaji kura kwa kiasi
kikubwa ulifanyika kwa amani huku kukiwa na misururu mirefu katika miji
nchini kote wakati wapiga kura wakipiga kura zao chini ya ulinzi mkali
takriban katika vituo 6,000.
Taliban imeukataa uchaguzi huo kuwa ni njama za kigeni na imewataka
wapiganaji wake kushambulia wafanyakazi wa uchaguzi, wapiga kura na
vikosi vya usalama.
Mkuu wa Tume Huru ya Uchaguzi (IEC), Ahmad Yusuf Nuristani ameliambia
shirika la habari la AFP kwamba watu wengi wamejitokeza kupiga kura
kuliko vile ilivyotarajiwa lakini hakutaja idadi bali amesema idadi hiyo
ni ndogo katika maeneo ya vijijini kulinganisha na mijini.
0 comments:
Chapisha Maoni
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.