Katika
siku za hivi karibuni, baadhi ya magazeti yamekuwa yakitoa taarifa za
upotoshaji juu ya suala la kuongezeka kwa malipo ya pensheni kwa
Waheshimiwa Wabunge. Magazeti hayo yanadai kwamba Mheshimiwa Waziri wa
Fedha amethibitisha ongezeko hili.
Taarifa hizo ziliendelea kudai kwamba Waheshimiwa Wabunge watakapostaafu watastahili kulipwa shilingi 160 milioni kila mmoja.
Kwa kupitia tangazo hili, tunaeleza kwamba, Mheshimiwa Waziri wa
Fedha hajawahi kuongea na Mwandishi wa Habari yeyote kuhusu suala la
nyongeza ya pensheni ya Waheshimiwa Wabunge na maelezo kwamba Mheshimiwa
Waziri alithibitisha taarifa za ongezeko hilo sio kweli bali ni maelezo
binafsi ya Waandishi wa Habari hizo na suala hilo halipo Serikalini
wala Bungeni.
Aidha, tunapenda kuwaasa Waandishi wa Habari kufanya kazi kwa
kuzingatia maadili ya taaluma yao na kuacha kuwachonganisha Wabunge na
Wananchi wanaowaongoza kwa kuwapotosha kwa masuala ambayo hayana ukweli
na uthibitisho wowote.
KATIBU MKUU – WIZARA YA FEDHA
4 FEBRUARI, 2014
4 FEBRUARI, 2014
0 comments:
Chapisha Maoni